Tuesday, 10 November 2015

KIPENZI MAMA

Miaka ni arubaini na fulani
Kila kukicha wazidi kupendeza
Mwenye upole bila fedheha
Kirembo chako kimekolea
Ukawa zaidi ya ua la waridi


Sala zako ni mafungulia ng’ombe
Jua lisichomoze bila Baraka zako
Imani yako imezidi ya bahari
Kina chake kimezidi kawaida
Lakini bado umejawa utulivu

Tabasamu lako la kufinyanga moyo
Ukarimu wako wa kutuliza majonzi
Hujabagua wala kupekua wanao
Kinywani pa mumeo umejaa
Sifa zako zimepita kileo cha dunia


Kipenzi mama
Miaka ni arubaini na Fulani
Wanao Umewalea bila kuchelea
Subiri Baraka zako
Zipo njiani hazitachelewa

5 comments:

  1. Subira huvuta heri kwani mama huyu kalea watoto wake akisubiri baraka. Hakuna baraka litakalozidi, baraka alichokipata alipojifungua kukuleta wewe (Desma) hapa duniani. *I tried*

    ReplyDelete
  2. Subira huvuta heri kwani mama huyu kalea watoto wake akisubiri baraka. Hakuna baraka litakalozidi, baraka alichokipata alipojifungua kukuleta wewe (Desma) hapa duniani. *I tried*

    ReplyDelete
  3. Heko dada kwa utunzi huu ulioshupavu, natumai Maulana yuatazama na hivi punde ombi lako litatimika. Kheri na fanaka kwa mama mzazi, inshallah!

    ReplyDelete
  4. hahahah Olave Orawo kweli umejaribu lakini usitie shaka kidogo kidogo utakipata ahsante kwa maoni

    ReplyDelete
  5. Paul natumai baraka zake tayari ashazipokea

    ReplyDelete