MAMANGU
by Desma Winnie Wood on Thursday, September 2, 2010 at 6:46pm ·
by Desma Winnie Wood on Thursday, September 2, 2010 at 6:46pm ·
Mamangu,
Unavyozidi kua
Dunia inabanduka
Nahofia waweza ukabanduliwa.
Wajua tena
Sipendi haya mambo
Ya kua mbali nawe .
Waelewa fika
Kama navyokupenda
Moyo si wangu
Maanake unakwenda mbali nami
Nenda chuo kasome
Mengine Mwenyezi Mungu atakujalia
Niskize mamangu tena kwa maakini
Babako ajivunia kisomo chako
Watu hapa mjini wamuonea ghere.
Mama usitutie aibu hata kuchao
Heshima ile niliyokufunza
Urejee nayo hapa kwangu
Mwanangu dunia rangi rangile
Kesho upakwe hili kisha lile
Bibie naomba ubakie hili rangi
Siku zako zote chuoni
Raha nyingi vilevi na hayo mengine
Yasikugeuze tusijekuelewa.
Mama nenda chuo soma.
Mchumba utampata baadaye
Usiwe mbioni
Msikize mwalimu
Heshima umpe ndio ufuzu
Mamangu nakupenda
Machozi yanikimbia viwili viwili
Sitoyapangusa mimi maanake
Wewe kipenzi changu
Umeona mengi tayari
Sioni mengine yapi watarajia
Fika pale soma pata cheti
Ufurahie yale alokupangia Rabuka
Nakupenda sana mwanangu
Mahuluki akujalie mahitaji yako yote
Kila kukicha.
Unavyozidi kua
Dunia inabanduka
Nahofia waweza ukabanduliwa.
Wajua tena
Sipendi haya mambo
Ya kua mbali nawe .
Waelewa fika
Kama navyokupenda
Moyo si wangu
Maanake unakwenda mbali nami
Nenda chuo kasome
Mengine Mwenyezi Mungu atakujalia
Niskize mamangu tena kwa maakini
Babako ajivunia kisomo chako
Watu hapa mjini wamuonea ghere.
Mama usitutie aibu hata kuchao
Heshima ile niliyokufunza
Urejee nayo hapa kwangu
Mwanangu dunia rangi rangile
Kesho upakwe hili kisha lile
Bibie naomba ubakie hili rangi
Siku zako zote chuoni
Raha nyingi vilevi na hayo mengine
Yasikugeuze tusijekuelewa.
Mama nenda chuo soma.
Mchumba utampata baadaye
Usiwe mbioni
Msikize mwalimu
Heshima umpe ndio ufuzu
Mamangu nakupenda
Machozi yanikimbia viwili viwili
Sitoyapangusa mimi maanake
Wewe kipenzi changu
Umeona mengi tayari
Sioni mengine yapi watarajia
Fika pale soma pata cheti
Ufurahie yale alokupangia Rabuka
Nakupenda sana mwanangu
Mahuluki akujalie mahitaji yako yote
Kila kukicha.
No comments:
Post a Comment